Na Gideon Mwakanosya,Songea
WAANDISHI wa habari wawili wawakilishi wa vyombo vya habari tofauti
mkoani Ruvuma wamefukuzwa kawenye ziara ya waziri mkuu wa Jamhuri wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda kwa kushutumiwa kuandika
habari ya ajali iliyotokea kwenye ziara hiyo wakati msafara wa waziri
mkuu ukitoka wilayani Tunduru kuelekea wilyani Namtumbo.
Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimethibitishwa na katibu
wa chama cha waandishi wa habari wa mkoa wa Ruvuma Andrew Chatwanga
zimeeleza kuwa tukio la kufukuzwa kwa waanahabari hao wawili limetokea
jana majira ya saa 1.45 katika eneo la Ikulu ndogo ya mjini Songea
wakati msafara huo unatarajia kuondoka kuelekea wilayani Nyasa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo waandishi wa habari wa mkoani
Ruvuma ambao walionyesha kushangazwa na tukio hilo la mwandishi wa
habari wa ofisi ya waziri mkuu Said Nguba kuwahoji kwa nyakati tofauti
wanahabari hao wawili kuhusiana na tukio la ajali iliyotokea juzi kwenye
ziara hiyo ya waziri mkuu ambayo ilisababisha magari manne kugongana na
kusababisha taharuki kwenye msafara huo huku baadhi yao kujeruhiwa.
Walisema kuwa mara baada ya ajali hiyo kutokea kulitolewa maelekezo na
Afisa habari wa mkoa wa Ruvuma Revokatus Ksimba mbele ya waandishi wa
habari waliokuwepo kwenye eneo la tukio kuwa taaifa hiyo ya ajali
isitangazwe kwenye vyombo vya habari kwa madai kuwa haina madhara
makubwa kauli ambayo ilipingwa pale pale na baadhi ya waandishi wa
habari .
Ajali hiyo ilihusisha magari manne yenye
namba za usajili PT 1437 Mali ya jesji la polisi,STK 7929,DFP 6627 na
DFP 8709 iliyokuwa imewabeba baadhi ya waandishi wa mkoa wa Ruvuma
pamoja na Afisa habari wa mkoa huo ambaye anadaiwa kuwa alipewa
maelekezo na baadhi ya waandishi wa habari waliotoka jijini Dar Es
Salaam pamoja na mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri mkuu ambao
walitoa maelekezo kuwa ajali hiyo ni ndogo na haina haja kuandikwa na
kutangazwa kwenye vyombo vya habari jambo ambalo baadhi ya waandishi wa
habari wa mkoa wa Ruvuma walilipinga kwa sababu wao ndiyo wahanga.
Katika ajali hiyo jumla ya waandishi habari nane wa mkoani Ruvuma
walikuwemo kwenye magari mawili kati ya magari manne yaliyopata ajali
hiyo iliyotokea kwenye kijiji cha Namingwea wilayani Namtumbo kwenye
msafara huo.
Hata hivyo katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma
Chatwanga alionyesha kusitikishwa na kitendo cha kuwafukuza waandishi
wawili ambao ni Nathan Mtega mwakilishi wa ITV na Radio One Stereo
mkoani Ruvuma na Ngaiwona Nkondola mwakilishi RFA na STAR TV Mkoani
Ruvuma ambao wanadaiwa kuandika na kutangaza habari za tukio hilo la
ajali iliyotokea wakati wao kama wanataaluma wa tasnia ya habari
wamehabarisha jamii yaliyojiri kwenye msafara huo.
Hata hivyo jitihada za kumpata mwandishi wa habari wa ofisi ya waziri
mkuu Nguba zimeshindikana kwa kuwa bado yuko kwenye msafara huo wa
waziri mkuu.
No comments:
Post a Comment