Na Mwandishi wetu, Tanzaniasasa
WAKUFUNZI wa vyuo vinavyotoa elimu ya uandishi wa habari nchini wametakiwa
kuwafundisha kwa ufasaha wanafunzi wao maudhui yaliyopo katika azimio Dar es
salaam kuhusu uwajibikaji na uhuru wa vyombo vya habari (DEFIR), ili kutengeneza
waandishi watakaofuata maadili ya habari na kuwa kioo kwa jamii.
Wito huo umetolea leo jijini hapa na Meneja utafiti na
machapisho wa Baraza la Habari nchini (MCT),
John Mirenyi katika warsha ya siku moja kuhusu azimio hilo kwa wakufunzi
na wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha (AJTC).
|
wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha, wakisoma maswali ya
tathmini ya warsha hiyo , picha na seif mangwangi wa tanzaniasasablog |
Mirenyi amesema taaluma ya habari imekuwa ikipokea waandishi
wengi kila siku jambo ambalo limekuwa likisababisha baadhi yao kuvunja maadili
ya uandishi wa habari na kuifanya kutoheshimiwa na jamii.
Amesema azimio la Dar
es salaam kwa wahariri , waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari (DEFIR)
limetoa mwongozo wa namna ambavyo waandishi wa habari wanatakiwa kufanya
shughuli zao ili kuijengea hadhi taaluma hiyo mbele ya jamii na kuifanya
kuheshimika kama zilivyo taaluma zingine.
|
Mwandishi Mkongwe na Rais wa chama cha waandishi wa habari za mazingira
JET Christom Rweyemam akitoa mada kuhusu azimio la wahariri jijini Dar
es salaam (DEFIR) katika semina hiyo |
|
Mwandishi Mkongwe na Rais wa chama cha waandishi wa habari za mazingira JET Christom Rweyemam akitoa mada kuhusu azimio la wahariri jijini Dar es salaam (DEFIR) katika semina hiyo |
|
Wakisikiliza kwa makini |
|
John Mirenyi Meneja utafiti na machapisho wa Baraza la Habari Tanzania (MCT0, akimtambulisha mmoja wa waandaaji wa semina hiyo ambae pia ni mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha |
|
Wakimsikiliza kwa makini mtoa mada |
|
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha AIJTC wakimsikiliza kwa makini mtoa mada (hayupo pichani). |
|
Wakufunzi na wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari Arusha, wakisoma maswali ya tathmini ya warsha hiyo , picha na seif mangwangi wa tanzaniasasablog |
|
Mhariri wa Radio Safina Lucas Daniel akisaini azimio la DEFIR |
No comments:
Post a Comment