Tuesday, June 4, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA RASIMU YA KATIBA MPYA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, VIWANJA VYA KARIMJEE DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiinua juu na kunyesha Kitabu cha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Asha-rose Migiro, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Makamu, ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd (kushoto) ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Rasimu ya Katiba mpya, Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, baada ya uzinduzi rasmi wa rasimu hiyo uliofanyika leo Juni 03, 2013 katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.  Katikati ni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Joseph Sinde Warioba.Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema (kulia) na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki, wakiperuzi kitabu cha Katiba mpya, baada ya kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, leo kwenye Viwanja wa Karimjee, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume ya Katiba mpya, baada ya uzinduzi huo.

BURUDANI kutoka kwa kundi la Mrisho Mpoto wakati wa uzinduzi wa Rasimu mpya ya Katiba



Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akiteta jambo na  mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba , Dkt Salim Ahmed Salim katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam jana

Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akiingia kwenye viwanja vya Karimjee katika hafla ya uzinduzi wa rasimu mpya ya Katiba, wa kwanza kulia mbele ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Warioba

Viongozi wa juu wa tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiwa wameketi meza kuu kusubiri shughuli za uzinduzi wa rasimu mpya ya Katiba kuanza

Viongozi wa kada mbalimbali Serikali na vyama vya siasa wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba

Viongozi mbalimbali wa Serikali wakimsikiliza kwa makini Jaji Warioba

Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akihutubia wananchi na viongozi mbalimbali waliojitokeza kwenye uzinduzi wa rasimu mpya ya Katiba

Waandishi wa habari wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa Tume Jaji Joseph Warioba

Waandishi wa habari pamojana wageni mbalimbali wakikisikiliza kwa makini hotuba ya mgeni rasmi

Makamu wa Rais Dkt Gharib Bilal akihutubia wananchi waliojitokeza kwenye hafla hiyo

No comments: