Mkurugenzi Msaidizi wa A TO Z Godwin George Abedi akizungumza na waandishi wa habari pichani jana |
Waandishi wa habari wakichukua habari |
A TO Z KUIFIKISHA RAI MAHAKAMANI KWA KUANDIKA HABARI YA UONGO
Na Seif Mangwangi
UONGOZI na Menejimenti ya kampuni
ya kutengeneza chandarua chenye dawa, A TO Z umekanusha taarifa zilizoandikwa
na gazeti moja la wiki (sio jamboleo), kuwa vyandarua hivyo vinatengenezwa
chini ya kiwango na havizuii mbu anaeambukiza ugonjwa wa malaria kutopenya.
Akizungumza na waandishi wa habari
jana jijini hapa, Mkurugenzi msaidizi wa kampuni hiyo, Godwin Abedi alisema
ubora wa chandarua hicho umehakikiwa na shirika la viwango nchini (TBS),
taasisi ya Malaria Ifakara, pamoja na mashirika makubwa duniani ikiwemo (WHO).
Alisema taarifa zilizochapishwa
katika gazeti hilo sio za kweli na kwamba zimeandikwa kwa lengo la kuchafua
kampuni hiyo na kuharibu shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na kampuni.
“Chandarua chetu kinatengenezwa
katika hadhi ya kimataifa, taarifa za kwamba hazina ubora si kweli kwa kuwa
hiki chandarua kabla ya kupakiwa na kusafirishwa kwa wateja kote duniani mashirika
ya viwango nchini kama TBS, (Ifakara Health Institute) na WHO wanavikagua
kuthibitisha ubora wake,”alisema.
Alisema kwa kuwa taarifa hiyo
iliyoandikwa haikuwa sahihi, wamekusudia kulishtaki gazeti hilo mahakama kuu
kanda ya Arusha na kwamba kupitia
kampuni ya uwakili ya Loomu Ojare and advocate ya jijini Arusha wameshamuandikia
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni inayomiliki gazeti hilo barua ya kusudio la
kulishitaki gazeti lake.
“Tumeshamuandikia mkurugenzi
mtendaji wa kampuni inayomiliki gazeti kusudio letu la kulishitaki gazeti lake kwa habari waliyoiandika ambayo sio ya
kweli, tumewapa siku 14 wakanushe habari waliyoiandika na kulipa hasara ambayo
imetupata,”alisema Wakili Loomu Ojare.
Alisema wamelazimika kufungua kesi
mahakama kuu bila kupitia baraza la habari nchini kwa kuwa kampuni hiyo imekuwa
ikifanya shughuli zake kimataifa na imekuwa na wabia wengi nje ya nchi
Kampuni hiyo imetuma barua yenye
kumbukumbu namba 42/MENH/MIS/LOC/2013 ya tarehe 8 Aprili 2013 kwenda kwa mkurugenzi
mtendaji New habari (2006), Limited
yenye kichwa cha habari ‘Demand letter for withdrawal and apology for
defamatory libel concerning A TO Z Textile mills limited published in RAI
newspaper of April 4 to April 10, 2013’.
No comments:
Post a Comment