|
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri wakisalimia |
ARUSHA
NA MWANDISHI WETU TANZANIASASA
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo amewataka wazazi
kutumia wiki ya chanjo kuwapeleka watoto kupewa matone dhidi ya magonjwa
mbalimbali ukiwemp wa Polio.
Ametoa kauli hiyo leo wakati wa uzinduzi wa chanjo watoto
walio chini ya umri wa miaka mitano mkoa wa Arusha katika Kijiji cha Mbuyuni
Kata ya Oljoro,wilayani Arumeru
Amewataka viongozi wa vijiji kuweka sheria ndigondogo
zitakazowabana wananchi ambao watakaidi kuwapeleka watoto kupata chanjo hiyo
muhimu inayogharimiwa na serikali kwa wananchi wake.
Mulongo amesema kutokana na chanjo hizo kutolewa baadhi ya
magonjwa yametoweka kabisa na zilizokuwa Wodi za magonjwa hayo katika hospitali
ya mkoa ya Mount Meru zinatumika kwa mambo mengine.
Awali Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha,Frida Mokiti alisema
mwitikio wa chanjo kwa mkoa wa Arusha unaridhisha kutokana na takwimu za mwaka
jana kuwa miongoni mwa mikoa minne iliyofanya vizuri kitaifa huku wilaya ya
Ngorongoro ikivuka asilimia 100.
Amesema utoaji wa chanjo hizo ni mkakati wa wizara ya Afya
na Ustawi wa Jamii kuhakikisha nchi inafikia lengo namba nnela millennia la
kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili sanjari na kuzitaka halmashauri
zote kufanikisha zoezi hilo kwa kiwango cha asilimia 95 kwa kila chanjo.
Kauli mbiu ya wiki ya chanjo kwa mwaka huu ni "Okoa Maisha.Kinga Ulemavu.Toa Chanjo
|
RC Magesa Mulongo akihutubia watu waliofika kwenye uzinduzi wa chanjo hiyo |
|
Kina Mama wakisubiri watoto wao kupewa chanjo |
|
Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Arusha,Thobias Mkina akisalimia
wananchi,Mkuu wa Mkoa(kushoto) na Diwani wa Kata ya Oljoro,Sanare
Miparali |
|
RC Mages Mulongo akihutubia wananchi waliohudhuria ufunguzi wa chanjo |
|
RC Magesa Mulongo akitoa chanjo |
|
Mkuu wa Mkoa Magesa Mulongo akifanya zoezi la kutoa chanjo kwa mmoja wa watoto waliohudhuria ufunguzi wa chanjo hiyo jijini Arusha |
|
Mkuu wa mkoa akitembelea mabanda ya maonesho na kupata maelezo |
|
Mtaalamu akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa |
|
Viongozi mbalimbali kutoka kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa wa
Arusha,Dk.Frida Mokiti,Katibu Tawala wa mkoa,Mama Itanisa na Mkuu wa
wilaya ya Arumeru,Nyirembe Munasa |
|
Oljoro safiiiii |
|
Chanjo oyeeeeee |
|
Oljoro safiiiiiiii? |
|
Mtaalamu akimweleza Mkuu wa mkoa jambo kuhusu mapambano dhidi ya ugonjwa
wa malaria kwa kutumia Vyandarua(katikati)Mganga Mkuu wa wilaya ya
Arusha,Thobias Mkina |
|
Akina mama wakiwa na watoto wao wakielekea kupata chanjo |
|
Akina mama wakiondoka kwa furaha baada ya watoto wao kupata chanjo ya Polio |
|
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo |
|
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha akizungumza kwenye uzinduzi wa chanjo ya Polio |
|
Mtaalamu akitoa maelezo kwa mkuu wa mkoa |
No comments:
Post a Comment