|
WAKIFUATILIA: waandishi wa habari wanachama wa APC wakifuatilia kwa makini mkutano wa dharura ulioitishwa na chama hicho, kushoto ni Daniel Sabuni, Cynthia Mwilolezi na Janeth Mushi |
ARUSHA
NA MWANDISHI WETU TANZANIASASA
Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Arusha(APC) kitafanya mkutano wake
wa mwaka ambao utawachangua viongozi wapya kushika nyazifa mbalimbali za
uongozi wa chama hicho.
Akizungumza mapema leo kwenye kikao cha dharula kilichokuwa na lengo ya
kupanga siku ya uchaguzi ambayo imekubaliwa kuwa ni Juni Mosi,mwaka
huu,Mwenyekiti wa APC,Claud Gwandu alisema ameita kikao hicho ili kuomba
ridhaa ya wananchama kupanga tarehe ya mkutano mkuu na uchaguzi
kutokana na kukabiliwa na maandalizi ya siku ya vyombo vya habari
itakayofanyika katika ngazi ya Kanda kwenye jiji la Arusha na
kuhudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200.
Alisema kikatiba uchaguzi ulitakiwa kufanyika mwezi Mei lakini kutokana
na kuwa APC ndio wenyeji wa siku ya vyombo vya habari imeonekana ni
busara kusogeza mbele siku ya mkutano mkuu ambayo itaenda sanjari na
kufanyika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa APC.
Kikao hicho kimewapitisha wajumbe watano watakaosimamia uchaguzi huo
ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na kila mwanachama
kuamini ana uwezo wa kuongoza akishirikiana na wanachama wenzake.
Katibu wa APC,Eliya Mbonea alisema mchakato wa kuandaa fomu
zitakazotumwa kwa wanachama utafanywa na kamati ya uchaguzi ambayo
wajumbe wake ni waandishi wakongwe,Willam Lobulu,Danford Mpumilwa,Mch
Amos Sekajingo,Zephania Ubwani na Kulwa Mayombi.
Baadhi ya wanachama waliozungumza na Blog hii hawakupenda kutaja nafasi
watakazowania kuwa ni mapema mno kutangaza na ni moja ya mbinu za
kisayansi kusaka ushindi.
Uongozi unaomaliza muda wake unajivunia mafanikio mbalimbali
yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuwa na ofisi ya kudumu,mafunzo ya
mara kwa mara,vitendea kazi na baadhi ya wanachama kulipa ada kwa
wakati.
|
MAJADILIANO: Mratibu wa APC, Seif Mangwangi wa pili kutoka kulia, Katibu wa APC Eliya Mbonea, mwanachama Richard Konga na Bertha Ismail wa kwanza kulia wakijadili jambo |
|
Makamu Mwenyekiti wa APC, Charles Ngereza pamoja na Anthony Masai wakionyeshana jambo kwenye komputa |
|
wanachama wakiendelea na kazi wakati mkutano ulipokuwa ukiendelea, aiyesimama nyuma ni Mustafa Leu, Veronica mheta na Cynthia Mwilolezi |
|
Mwanachama wa APC, Veronica Mheta akiuliza swali katika mkutano huo |
|
Katibu mkuu wa APC Eliya Mbonea akisoma agenda za mkutano huo, kulia kwake ni Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu |
|
MAAKULI: waandishi wa habari wakipata chai katika mkutano huo, wa kwanza kushoto, MC Kassim Kiko, Edward Selasini, Abraham Gwandu, Magesa Magesa, Cynthia Mwilolezi na Richard Konga |
|
Viongozi wa juu wa APC, Charles Ngereza kushoto, Claud Gwandu katikati (Mwenyekiti) na Eliya Mbonea (Katibu Mkuu) wakiteta jambo katika mkutano huo |
|
Mwenyekiti wa APC akijibu hoja |
|
Waandishi wa habari Cynthia Mwilolezi na Janeth Mushi katika picha ya pamoja |
|
Mwandishi Mkongwe na mjumbe wa kamati ya utendaji David Frank akiperuzi gazeti la Mwananchi |
No comments:
Post a Comment