Na Mwandishi Wetu
Mwenyekiti General
Ulimwengu,aliwahi kusema `Raia Mwema ama Raia Muungwana ni Yule anayeamka
asubuhi na kujiona ni mwenye afya njema ,kisha anampigia simu daktari wake na
kumuuliza hatma ya afya yake kwa miaka mitano ama kumi ijayo.(Ntafafanua).
Nimekuwa mmoja wa `waumini`
wazuri wa gazeti la Raia Mwema kwa muda mrefu sasa,nemepata mengi na kujifunza
mengi kupitia makala mbalimbali zinazopewa nafasi katika gazeti hili hasa kwa
Makala zinazoandikwa na Waandishi waliyobobea kama Johnson Mbwambo ambaye
ameanza `kuzeeka vibaya`.
Toka nipo Shule ya Msingi na
Mpaka sasa nimekuwa Mwanahabari Bado namsoma Mzee Mbwambo ambaye kwangu
nilimuona kama Mwalimu Wangu wa siku nyingi sana bila yeye kujijua,lakini hivi
karibuni amenifundisha somo ambalo si tu sijalipenda bali pia sijapata jibu
kama Mwalimu Wangu alikuwa `amelewa` wakati anaandika ama alikuwa ametanguliza hasira za kunyimwa Ukuu
wa Wilaya mbele!!!
Katika Raia Mwema Toleo na.292 la
April 30,ukurasa wa 11 Kuna Tafakuri
Jadidi Iliyoandikwa na Johnson Mbwambo.Ina kichwa Kikubwa cha Habari kinasema
KIKWETE KAWASIFU,SASA WANASHINDANA KUITUKANA CHADEMA! Nimesoma kilichoandikwa
na Mwalimu Wangu nikapata shaka na anapoelekea `kiumri`.
Kwakawaida Binadamu kadiri
unapoongezeka Umri na ndivyo Busara zinavyoongezeka na ndiyo maana kukawa na
msemo usemao `Utu uzima ni dawa`.Mimi ni mmoja wa wanaoamini Mbwambo
anaongezeka Umri na siyo urefu,kidogo Napata shaka kuamini kama ongezeko lake la umri linakwenda sambamba na
ongezeko la busara.
Mbwambo amekuwa mshabiki kiasi
cha kupitiliza,na kwa kiwango hicho ameshindwa kuthibiti hasira zake na
kujitofautisha na hao wabunge wanaotoa lugha `chafu` nayeye ametumbukia humo
huku `akijifanya kutumia mgongo wa falsafa za Mwalimu Nyerere.
Katika Makala iliyotoka katika
gazeti hili Mbwambo kama kawaida yake ametumia muda mwingi kuwashambulia
Wabunge vijana wa chama cha Mapinduzi
kwa madai `eti` wamekuwa wakikikejeli chama chake cha Chadema Bungeni
badala ya kuongea mambo ya Msingi.Akasema `eti`wamekuwa wakiwafanya hata
Wabunge wa `chama chake ` cha Chadema kujibu kwa Ukali( hakuita ni matusi) eti
kwasababu ya Wabunge vijana wa ccm wanaotukana.( ya CCM akaita matusi)
Akiendelea kuandika makala yake
Mbwambo kila mara amekuwa akijikingiliza
katika kimvuli cha Mwalimu Nyerere `kinafiki`kujaribu kuhalalisha maandishi yake yakukitetea chama chake
kinachodaiwa kuwa na `udini na ukanda`( Mwambo anatokea Kilimanjaro)
Mbwambo katika maandishi yake
akasema (namnukuu) ``Isitoshe,Chadema kiumri si chama kikongwe kama ccm na
hivyo katika hali ya kawaida wabunge wa ccm ndiyo wanaopaswa kuonyesha mfano wa
uungwana Bungeni kwa wabunge wa Chadema kwakuwa wao wanatoka katika chama
kikongwe na kinachokamata serikali kwa miaka mingi`` ( mwisho wa kunukuu) ``Mzee Mbwambo anamaudhi sana`.
Kwa maandishi yake anataka kutufundisha
kuwa wabunge wa Chadema wakitukana tuwaunge mkono kwakuwa wapo katika chama
kichanga wala wasikosolewe, na Kwakuwa Chama chao hakishiki Dola basi waachwe
tu waporomoshe matusi kama wanavyofanya sasa!!
Yaani Mbwambo anataka Wabunge wa
ccm wawe wavumilivu kuvumilia `upuuzi ` wa wabunge wa Chadema . Sitaki kuamini
kama Kule kwao Kilimanjaro mtoto akitukana anaachwa kwakuwa bado mdogo ( labda
anafanya hivyo kwake) Ndiyo maana Napata shaka na umri wa Mzee Mbwambo
unapoelekea! Katika makala yake Mbwambo ameongea mengi yanayokera `kama yeye
alivyokerwa na Yule mwandishi aliyemwita `mhandisi anayempigia debe Babu wa
Loliondo eti Dawa zake ni tiba sahihi`.
Katika kuifanya Jamii izidi
kuiamini taaluma ya Uandishi wa habari ni lazima sisi waandishi wa habari bila kujali mkongwe ama mchanga tusiwe
makatibu waenezi wa vyama vya siasa.
Katika Maandishi yake Mbwambo anaandika kama vile siyo
mwandishi wa habari bali ni `Mwajiriwa wa Chadema`.
Siku zote nimekuwa nikimsoma
Mbwambo na kumwelewa na kujifunza kwa kile anachokiandika lakini kwa hili
nimeshindwa kuingiza ndani ya ubongo wangu `ushawishi wake` usiyofaa mbele ya
jamii kuwa eti watukane wa Chadema,lakini ccm hapana.
Binafsi siungi mkono lugha chafu zinazotolewa na baadhi ya
wabunge bila kujali vyama vyao,sipendi kuona wabunge wanakuwa kichaka cha
matusi kwa sisi vijana ama watoto wadogo zaidi yangu kwa namna yeyote ile.
Mbwambo amejielekeza zaidi
kuiaminisha jamii kuwa yanayotolewa na Chadema siyo matusi bali ni hoja za
msingi na yanayotolewa na baadhi ya wabunge wa ccm siyo majibu ama hoja bali ni
matusi.
Mzee Mbwambo amefika mbali zaidi
kwa kudai kuwa baadhi ya wabunge wa CCM
wamesifiwa na Rais Jakaya Kikwete na ndiyo maana wamezidi kutukana
matusi
Akasema Mwigulu Nchemba alipewa
zawadi ya cheo baada ya kukitukana Chadema
na ndiyo maana basi wengine wanaiga ili wapewe zawadi ya vyeo.
Anavyoamini yeye (Mbwambo) CCM
wakichaguana katika chaguzi zao kama Chadema basi ni kupeana zawadi za vyeo na
siyo haki, CCM wakiteuana kulingana na katiba yao kwa mtazamo wa Mzee Mbwambo
huo siyo uteuzi ila ni zawadi baada ya kutukana!
Mzee Mbwambo ameondoka katika
uandishi na kuwa mtu wa Propaganda wa Chadema,sitaki kuamini kama kuna
mwandishi anayefuata misingi ya taaluma anaweza kuwa na upendeleo kiasi hicho.
Inawezekana kabisa alichokiandika
Mzee Mbwambo ni Mawazo yake. Lakini mawazo gani hayo yanayowaza upande mmoja
pake yake,mawazo gani ambayo hubadilisha `matusi` kuwa maneno matamu?
Mawazo gani hayo nayaona matusi
ya wabunge wa chadema kuwa ni maendeleo?
Huu ni umbilikimo wa fikra ambao hauendi sambamba na heshima alonayo Mzee
Mbwambo.
Mzee Mwambo aliwahi kumshambulia
Mwandishi mmoja mkoani Arusha akimwita `Mhandisi wa habari` kwa kuwa mwandishi
huyo aliandika habari zinazomhusu Babu wa Loliondo na Mwandishi huyo
hakuonyesha kuiaminisha jamii kuwa dawa za Babu hazifai.
Alimshambulia mwandishi na
kumwelekeza kuwa ni afadhali angeandika habari hiyo kwa mtindo wa kukejeli ili asionekane kushabikia ushirikina wa Babu.
Sasa Mzee Mbwambo alichokiandika
yeye ni afadhali ya huyo Mwandishi aliyemwita `Mhandisi`.
Ameshabikia upuuzi wa baadhi ya
wabunge hasa wa chadema,na siwezi kumwita yeye ni `mhandisi`.
Waandishi jamii ya Mzee Mbwambo
huko tuendako ni hatari kwa kizazi cha taaluma ya habari.Atawaambukiza ushabiki
waandishi wachanga na wanaomsoma ambao watakuwa ni wavivu wa kutafakari kama
anavyomaliziaga makala zake kwakusema tafakari.
Binafsi nimetafakari nimebaini
umendika kiushabiki,na kama siyo kiushabikia basi pengine unaweza kuwa na una
hasira na Rais Kikwete,labda hukupata ukuu wa wilaya nk.tafakari mwenyewe.
Raia Mwema ni Yule anayeamka
asubuhi na kujiona ni mwenye afya njema lakini anampigia simu daktari wake
akimuuliza hatma ya afya yake miaka kumi ijayo.
Mzee Mbwambo ameamka asubuhi
amejiona ni mwenye afya njema,hampigii daktari wake simu anadunda tu barabarani
hajui madhara ya baadaye.
Angempigia daktari wake simu
angeambiwa maradhi yako ya fikra yanaambukiza hivyo usisambaze maradhi yako ya
fikra za upande mmoja kwa watu wote hasa kwa sisi vijana tunaokuwa katika
maadili mazuri.
Tafakari…O752 25 01 57…// 0655
2501
No comments:
Post a Comment