Sunday, February 2, 2014

MBUNGE NAMELOK SOKOINE AGAWA MISAADA KWA KITUO CHA WALEMAVU MONDULI, ATOA WITO

Mbunge wa Viti maalum Namelok Laizer akimjulia hali mtoto mwenye ulemavu wa utindio wa ubongo kituo hapo
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akiwasili kwenye kituo cha watoto yatima Monduli tayari kwa kutembelea wagonjwa na kugawa misaada
Mmoja wa watoto walemavu katika kituo cha walemavu cha Monduli akikabidhiwa mpira na mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine
Namelok akimkabidhi msaada wa ndoo ya sabuni mratibu wa kituo cha watoto walemavu Monduli Mireile Kapilima katikati ni Katibu wa UWT Mkoa wa Arusha Stamili Dendegu
Mratibu wa kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Monduli Mireile Kapilima akiwa amebeba moja ya ndoo ya sabuni aliyokabidhiwa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Arusha Namelok Sokoine
Mbunge Namelok Sokoine akimkabidhi mratibu wa kituo cha watoto walemavu Monduli Mireile Kapilima moja ya mablanketi aliyoyaleta kama msaada kwa kituo hicho
Mbunge wa viti maalum Namelok Sokoine akimjulia hali mmoja wa watoto wenye ulamavu wa miguu kituoni hapo
mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Namelok Sokoine akimjulia hali mmoja wa watoto wenye ulemavu wa mtindio wa ubongo katika kituo cha kulelea walemavu kilichopo Monduli jijini Arusha


Na Seif Mangwangi, Monduli

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, juzi Katibu wa umoja wa wanawake wa CCM (UWT), Mkoa wa Arusha Stamili Dendegu alijikuta akitokwa machozi baada ya kupata taarifa ya mahitaji muhimu yanayokikabili kituo cha kulelea watoto yatima waliopasuliwa miguu na kunyooshwa kufuatia kuzaliwa wakiwa walemavu.

Katibu huyo aliyekuwa akimribisha Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha Namelok Sokoine aliyetembelea kituo hicho cha walemavu kilichopo Monduli kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo la Arusha, alisema watoto hao wanahitaji kupata msaada mkubwa kutoka kwa watanzania wote na sio kuliachia kanisa pekee.

“Jamani tuwaonee huruma hawa watoto, na wale watoto waliokuwa majumbani ni vyema wakaletwa hapa wapate msaada, hata hivyo kituo kinakabiliwa na uhaba wa fedha za kujiendesha inatia uchungu sana, ndugu zangu tujitokeze kusaidia hawa watoto kwa fedha na mahitaji mengine,”alisema huku akitokwa machozi.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi iliyoenda sanjari na ugawaji wa misaada mbalimbali ya kibinaadam, Namelok Sokoine alisema kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na upungufu wa fedha za kujiendesha jambo ambalo limeulazimu uongozi wa kituo kuwatoza wazazi wa watoto wanaofikishwa kituo hicho sh1500 kwa siku.

“Disemba mwaka jana nilitembelea hiki kituo na kukuta tatizo kubwa wanalokabiliana nalo ni ukosefu wa ufadhili na kulazimika kuwatoza wazazi wa watoto wanaoletwa kwa matibabu hapa Tsh1500, kihalisia ni fedha ndogo lakini kwa hali duni za wazazi ni fedha nyingi sana na ndio maana leo nimetembelea hapa kuleta msaada kidogo,”alisema.

Alisema ni wakati sasa wa kila mtanzania kujiona ni mwenye jukumu la kusaidia yatima na wasiojiweza ili waweze kupata mahitaji muhimu ikiwemo fedha za matibabu na kuwaondolea hali ya ulemavu waliyokuwa nayo.

Awali akitoa taarifa ya kituo hicho, Mratibu wa kituo Mireile Kapilima alisema kituo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa ufadhili na kwamba mahitaji yamekuwa mengi kulingana na uwezo wa kituo ambapo hivi sasa kinalaza wagonjwa 52 huku uwezo wake ikiwa ni kulaza watoto 30.

Misaada mbalimbali ilitolewa jana na mbunge Namelok ni pamoja na Blanketi kwa ajili ya kujifunika, unga, sabuni, mafuta ya kupikia na fedha.