Wednesday, September 18, 2013

WAZIRI MAGHEMBE AINUSURU POLISI ARUSHA KUKATIWA MAJI KWA DENI LA MIL300

Wafanyakazi wa Mamlaka ya maji Arusha (AUWSA) wakimsikiliza waziri maghembe 

Mkurugenzi wa AUWSA Injinia Ruth Koya akiwasilisha taarifa ya AUWSA mbele ya waziri wa maji Jumanne Maghembe 

Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akizungumza na wafanyakazi pamoja na bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya maji Arusha AUWSA 

Waziri wa maji Jumanne Maghembe akizindua bodi ya mamaka ya maji jiji la Arusha (AUWSA)

Waziri wa Maji Jumanne Maghembe akimkabidhi nyaraka za mamlaka ya AUWSA Mwenyekiti mpya Felix Mrema 

Waziri wa maji Jumanne Maghembe akimkabidhi mwenyekiti wa bodi ya AUWSA Felix Mrema zawadi 

Makamu Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya maji ya AUWSA Anold Kileo akipokea zawadi ya utendaji bora wa bodi iliyopita kutoka kwa waziri wa maji Jumanne Maghembe

NA MWANDISHI WETU, TANZANIASASA
WAZIRI wa maji Professa Jumanne Maghembe juzi alilazimika kuingilia kati na kuiagiza Mamlaka ya maji jiji la Arusha (AUWSA), kusitiza zoezi la kuwakatia maji wadaiwa sugu taasisi za Serikali ikiwemo jeshi
la Polisi Arusha linalodaiwa deni la maji milioni 308.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa bodi mpya ya wakurugenzi wa mamlaka hiyo, Waziri Maghembe aliiagiza mamlaka hiyo kumwachia jukumu la kuzungumza na viongozi wa mamlaka za Serikali zinazodaiwa na mamlaka hiyo.

Waziri Maghembe alisema Mamlaka za maji nchini zinakabiliwa na changamoto kubwa ya upotevu wa mapato ikiwemo kupotea kwa maji kwa asilimia 38 ya maji yote yanayozalishwa na mamlaka hizo  na
kusababisha upotevu wa bilioni2 kwa kila mwezi.

 “Nawaomba hili suala la Mamlaka za Serikali kudaiwa mniachie nipambane nalo kwanza msiwakatie maji mpaka nitakapoonana nao, lakini pia hakikisheni mnapambana na changamoto zingine kama vile kuongeza
ukusanyaji wa mapato hadi kufikia asilimia 100 kutoka asilimia 93 mliyokuwa nayo hivi sasa,”alisema.

Waziri Maghembe pia aliiagiza bodi ya mamlaka hiyo kushirikiana na mamlaka za Mkoa na Wilaya za Arusha kutafuta vyanzo vipya vya maji na kuvihifadhi ili kusaidia upatikanaji wa maji kwa miaka ijayo wakati
vyanzo vilivyopo hivi sasa vitakapokauka.

“ Utafiti unaonyesha eneo la viwanja vya burka hadi Ngaramtoni ndio kuna maji mengi chini lakini badala ya kuchukua viwanja na kuvitunza kwa ajili ya baadae nyie mmeuza viwanja watu wanajenga maghorofa, hii
sio sahihi kabisa, bodi nawaagiza mtafute viwanja katika eneo hilo kwa ajili ya vizazi viavyo pindi maji yatakapopungua hapo baadae katika maeneo ambayo mnatumia hivi sasa,”alisema.

Awali Mwenyekiti wa bodi ya mamlaka hiyo mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha, Felix Mrema aliigiza menejimenti na  wafanyakazi wa mamlaka hiyo kufanyakazi kwa malengo ili kujiongezea mapato na wao kupata maslahi mazuri.

“  Endapo mtakusanya mapato ya kutosha na kutokomeza tatizo la upotevu wa maji ambalo ni zaidi ya bilioni mbili hivi sasa basi  na nyie mtapata mshahara mzuri kwa kuwa fedha itakuwepo, na kwa taarifa yenu sisi tunalipata mshahara kutokana na makusanyo tunayoyafanya, hivyo
fanyeni kasi kwa kazi ili mapato yaongezeke,”alisema Mrema.

Awali katika taarifa yake, Mkurugenzi wa mamalaka hiyo Injinia Ruth Koya alisema AUWSA kwa kushirikiana na wizara ya Maji imetenga bajeti ya bilioni 1.98 kwa mwaka wa fedha 2013/14 kuongeza usambazaji wa maji kwa kuchimba visima virefu na ujenzi wa tenki katika maeneo ya Sokoni1, Moshono, Olasiti, na Esami.

No comments: