Monday, April 29, 2013

MBUNGE LEMA AACHIWA KWA DHAMANA YA MILIONI MOJA, APANDISHWA KIZIMBANI KWA MADAI YA KUMKASHIFU RC MULONGO KWA MANENO KWAMBA 'ANATEMBEA KAMA ANAENDA KWENYE SENDOFF'

wafuasi wa CHADEMA wakimsikilia Lema

Wafuasi wa CHADEMA wakimsikiliza Mbunge wao Godbless Lema alipokuwa akiwahutubia leo katika viwanja vya shule ya msingi ngarenaro

wafuasi wa chadema wakiwa wamezingira viwanja vya mahakama kuu jijini hapa
Mama mmoja shabiki wa CHADEMA akionyesha bango lenye maandishi kuonyesha hisia zake kwa Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.

Umati wa mashabiki wa CHADEMA jimbo la Arusha wakimsikiliza mbunge wao Godbless Lema baada ya kutoka mahakamani, hapa akiwahutubia wananchi hao katika viwanja vya shule ya msingi Ngarenaro pembeni ya ofisi ya Chadema Mkoa wa Arusha

Mbunge Lema pamoja na Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua nasari wakiwa juu ya gari wakihutubia umati wa wananchi waliojitokeza baada ya kupata dhamana kwa kosa la kukashifu
Kwa mujibi wa waendesha mashtaka wa Serikali, Mambo yaliyomfanya Mbunge wa arusha Godbless Lema akamatwe na kunyimwa dhamana  ni haya yafuatayo;

i)Kosa la kwanza ni kuwaambia wanafunzi wa chuo cha uhasibu alipoenda kuwatuliza kuwa ‘dhambi kubwa kuliko zote ni woga ‘. Haki hutafutwa na kupiganiwa ikiwa jambo unalipigania ni la msingi na linafaa kupiganiwa (Worth fighting for)

ii)Kosa la pili ni pale alipotamka kuwa ‘’Tumemtafuta mkuu wa mkoa juu ya Matatizo yenu na mlivyoshuhudia hapa amechukua muda mrefu na kuingia kama vile anaingia kwenye send-off.Hawa ndiyo viongozi wetu ambao hawajali matatizo ya wananchi’’
iii)Kosa la Tatu ni pale alipotamka kuwaambia wanafunzi kuwa ‘’Mimi Mbunge wenu nipo sambamba nanyi hadi mpate haki yenu na ikiwa mkuu wa mkoa hatakuja hapa kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi wa mkoa nitawaongoza hadi ofisini kwake ili mpate majibu na haki yenu kwani ni haki yenu ya msingi kwa mujibu wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo niliapa kuilinda Bungeni na pia inaruhusiwa kwa mujibu wa kikanuni na kifalsafa katika utekelezaji wa utawala bora wa kidemokrasia ambao msingi wake ni kusikilizwa na kulinda haki za binadamu’’

No comments: