Thursday, April 11, 2013

PICHA MBALIMBALI ZIKIONYESHA MAJENGO YA KITUO CHA USHURU WA PAMOJA KATIKA MPAKA WA HOLILI YANAYOTARAJIWA KUANZA KAZI HIVI KARIBUNI

Jengo litakalokuwa likitumika na nchi za Tanzania na Kenya katika mpaka wa Holili kwa ajili ya shughuli za uhamiaji na ushuru wa pamoja. jengo kama hili pia linajengwa kwa upande wa Kenya ambapo pia maofisa wa pande zote mbili watakuwepo

Ujenzi wa jengo lingine litakalotumika kwa shughuli za ushuru ukiendelea mpakani Holili

Waandishi wa habari kutoka nchi za Kenya na Tanzania wakimsikiliza Ofisa katika mpaka wa Holili akitolea maelezo ujenzi unaoendelea mpakani humo

Waandishi wa habari wakiwa upande wa Tanzania mpaka wa Holili wakiangalia mandhari ya upande wa Kenya

Mafundi wanaojenga daraja linalotenganisha mpaka wa Kenya na Tanzania wakiwa kazini, hapa mmoja wa mafundi hao wanaojenga pia barabara mpakani hapo akikimbilia wenzake (hawaonekani pichani), huku waandishi wa habari wakishuhudia kwa mbali

Mkurugenzi wa Blogu hii Seif Mangwangi, wa pili kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wageni kutoka nchini Kenya, wa kwanza kulia ni Afisa katika mamlaka ya kodi nchini Kenya na anayefuatia Mwanamke ni mhitimu wa mafunzo ya clearing and forwading nchini Kenya

Mkurugenzi wa blogu hii Seif Mangwangi  akibambia katika kunogesha utamu wa picha

Kibao hiki kipo Taveta nchini Kenya, kinaonyesha sehemu ambayo malazi yanaweza kupatikana kwa wale wageni katika eneo hilo

Waandishi wa habari kutoka Kenya na Tanzania wakirandaranda mtaani katika mji wa Taveta walipoamua kutembelea mji huo baada ya kumalizika kwa mkutano na maofisa wa chuo cha clearing and forwading uliokuwa ukifanyika katika hoteli ya Mountmeru hivi karibuni

KIJIWENI: Baadhi ya wakazi wa mji wa Taveta wakiendelea na shughuli zao za kila siku

No comments: