Thursday, April 18, 2013

PICHA MBALIMBALI UFUNGUZI WA MAFUNZO KUHUSU MTENGAMANO WA AFRIKA MASHARIKI KWA WATENDAJI WA HALMASHAURI ZA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI KATIKA HOTELI YA NAURA JANA

Mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo

PICHA YA PAMOJA

PICHA YA PAMOJA

PICHA YA PAMOJAMkuu wa Wilaya yaMonduli Jowika Kasunga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Halmashauri za wilaya za Mkoa wa Arusha

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Kilimanjaro

Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na watendaji wa Halmashauri za wilaya za Mkoa wa Manyara

Mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akijbu maswali ya waandishi wa habari

Mkuu wa Wilaya ya Monduli Jowika Kasunga akijibu maswali ya waandishi wa habari pichani

Naibu Katibu Mkuu wizara ya ushirkiano wa Afrika Mashariki Uledi Mussa akijbu maswali ya waandishi wa habari

WAANDISHI KAZINI: hapa wanonekana wakimhoji Naibu Katibu Mkuu Uledi Mussa

Naibu Katibu Mkuu wizara ya ushiriano wa Afrika Mashariki Uledi Mussa akizungumza na waandishi wa habari
TANZANIA YATAKIWA KURUHUSU MAHINDI KUUZWA KENYA

Na Seif Mangwangi, Arusha

TANZANIA imekuwa ikikosa fedha nyingi za kodi kufuatia wafanyabiashara
nchini kutumia njia za magendo mipakani maarufu kama ‘ Panya road’
kusafirisha mazao yao hasa Mahindi kwenda nchi jirani kufuatia kuzuiwa
kusafirisha mazao hayo.

Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
ushirikiano wa Afrika Mashariki, Uledi Mussa wakati wa ufunguzi wa
Mkutano wa siku tano kwa maafisa waandamizi wa Halmashauri za wilaya
za Mikoa ya Kanda ya Kaskazini kuhusu mtangamano wa Afrika Mashariki.

Mussa alisema ili kuepukana na tatizo hilo Tanzania inatakiwa kuruhusu
uuzwaji wa mazao yake katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki ili kuimarisha uhusiano wa nchi hizo pamoja na kuwapatia
soko zuri wakulima wake na kuiingizia Tanzania fedha nyingi za kodi.

Alisema endapo nchi wanachama zitaruhusu uuzwaji wa bidhaa hizo,
wananchi wake watapata fursa ya kuongeza uzalishaji kwa kuwa watakuwa
wakifahamu soko zuri ambalo watakuwa wakipeleka bidhaa zao na hivyo
kuwapa hamasa ya kuliza zaidi.
Mussa alisema kuwakataza wananchi kuuza mazao yao nchini Kenya na nchi
zingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kumekuwa
kukisababishia Tanzania hasara kufuatia wananchi hao kutumia njia za
magendo maarufu ‘panya road’ kusafirisha mazao yao.

“ Tanzania imekuwa ikikataza wananchi wake kuuza zao hasa la Mahindi
nchini Kenya, hili bado sio jambo zuri kwetu kwa kuwa endapo watauza
mazao haya na kupata soko zuri, itawatia moyo wananchi na kulima kwa
wingi zaidi, hivi sasa watumia panya road na kuikosesha nchi mapato
mengi, kuwazuia sio suluhisho,”alisema.

Awali akifungua mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa ushirikiano wa
Afrika Mashariki Samwel Sitta, Mkuu wa Wilaya ya Monduli Jowika
Kasunga aliwataka Wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya nchini nchini
kuanzisha madawati maalum yatakayokuwa yakitoa elimu kuhusiana na
fursa zinazopatikana kwenye Jumuiya hiyo.

Sitta alisema Jumuiya ya Afrika Mashariki imekuwa na fursa nyingi
ambazo zikitumiwa vizuri zitawakomboa wananchi wa Tanzania kiuchumi
lakini kutokujulikana kwa fursa hizo kumewafanya wananchi wengi
kupuuzia Jumuiya hiyo.

“ Jumuiya ya Afrika Mashariki ina fursa nyingi lakini wananchi
hawazijui kutokana na ukweli kwamba taarifa zake hazijulikani kwa kuwa
hakuna wa kufanya hivyo, ningependa kutoa wito kwa wakurugenzi kutumia
wataalam wenu kutoa hizi taarifa kwa wananchi kwa kuanzisha madawati
hayo,”alisema Sitta.

Sitta alisema mbali na fursa mbalimbali ambazo zimekuwa zikipatikana
katika Jumuiya hiyo, pia kuna changamoto nyingi ambazo hata hivyo
wanaopaswa kuzitatua changamoto hizo ni watendaji kupitia Halmashauri
za Wilaya nchini.
Ends…

No comments: