Sunday, June 23, 2013

MKURUGENZI TANZANIASASA BLOG ACHAGULIWA KUWA KATIBU MKUU WA APC, WAJUMBE WAMPA KURA ZA NDIO 32 KATI YA 36, NI BAADA YA KUKOSA MSHINDANI

Katibu Mkuu anayemaliza muda wake Eliya Mbonea kushoto akisikiliza hotuba ya ufunguzi ya Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu

Baadhi ya viongozi waliomaliza muda wao na wengine baadhi yao kuchaguliwa kutoka kushoto ni Frank David, Mosses Kilyinga aliyekuwa katibu msaidizi na kukosa baada ya kushindwa na Mustafa Leu kwa zaidi ya kura kumi, Mary Mwita aliyemaliza muda wake na hakutetea tena nafasi hiyo, Eliya mbonea aliyemaliza muda wake na hakutetea tena nafasi hiyo 

Aliyekuwa katibu mkuu wa APC Eliya Mbonea akisoma taarifa ya utekelezaji ya miaka mitatu ya chama hicho tangu uongozi huo ulipoingia madarakani 2010
Mmoja wa wakurugenzi wa Blog hii Semmy Kiondo na KATIBU Mkuu wa APC  katika picha ya pamoja na viongozi wenzake wateule waliochaguliwa na wanachama katika uchaguzi mkuu uliofanyika hoteli ya Olasiti jijini hapa jana wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jamiiblog Pamela Mollel aliyechaguliwa kuwa Mwekahazina na katikati ni Janeth Mushi aliyechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji

Mmoja wa wajumbe na wanachama wakongwe wa APC John Mhala akisalimiana na aliyekuwa mwekahazina wa APC aliyemaliza muda wake Mary Mwita katika viwanja vya olasiti Gardena jana mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa chama hicho , kushoto ni Daniel Sabuni

kutoka kushoto Deus Buganywa msimamizi wa uchaguzi, Semmy Kiondo (KATIBU MKUU), Claud Gwandu (MWENYEKITI), na Charles Ngereza (MAKAMU MWENYEKITI)

Katibu Mkuu wa APC na ambae ni mmoja wa wakurugenzi wa Blog hii Semmy Kiondo akichangia taarifa ya fedha kwenye mkutano mkuu wa APC katika ukumbi wa Olasiti Garden jana

Semmy kiondo wa pili kutoka kushoto waliokaa katika picha ya pamoja na viongozi wapya wa APC

Mmoja wa wakurugenzi wa Blog hii Semmy Kiondo wa pili kutoka kushoto waliokaa katika picha ya pamoja wa kwanza kushoto ni aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi ambae ni mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya UTPC Deus Buganywa, Mwenyekiti Claud Gwandu na Makamu Mwenyekiti Charles Ngereza, nyuma ni wajumbe  na wanachama wa APC

Mwenyekiti mpya Claud Gwandu aliyetetea kiti chake akitoa salamu za pongezi kuchaguliwa kwa uongozi mpya, wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa blog hii Semmy Kiondo na wa mwisho ni Makamu Mwenyekiti Charles Ngereza ambae na yeye pia alitetea nafasi yake

No comments: